Jumla ya watoto saba mayatima wenye umri wa kati ya miaka 11 na 18 kutoka mjini Nambale Kaunti ya Busia wanaishi maisha ya mahangaiko baada ya mama mzazi kuwatoroka zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Watoto hao ambao baba yao aliaga dunia mwaka 2013 na kuzikwa katika makaburi ya Busia sasa hawana sehemu ya kuita nyumbani wala mzazi baada ya mama yao kwa jina Agnes Wesonga kuwatoroka mwaka 2018.

Baada ya kufurushwa katika chumba walichokuwa wamepanga, watoto hao wamekuwa wakikesha nje hadi walipopata msamaria aliyewapa sehemu ya kulala, wakitegemea chakula cha msaada.

 Kwa sasa wito umetolewa na viongozi wa akina mama eneo hilo wakimshauri mama mzazi kuwarejelea wanawe ili washirikiane katika malezi ya watoto hao ambao baadhi yao wamesitisha masomo ili kuwatafutia wadogo wao chakula.

Story by Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE