Jumla ya wauguzi na wahudumu wa afya 22 katika zahanati ya Khamulati eneo bunge la Kimilili wamewekwa karantini ya siku 14 baada yao kutangamana na mgonjwa aliyepatikana na virusi vya Korona na baadaye kufariki dunia kutokana na ugonjwa Covid-19 akitibiwa katika hospitali ya kibinafsi ya Life Care mjini Bungoma.

Kwa mujibu wa Mshirikishi wa magonjwa ibuka kaunti ya Bungoma Moses Wambusi, idara ya afya kwenye kaunti ya Bungoma ilichukua hatua ya kuwaweka karantini wahudumu hao wa afya ikizingatiwa kuwa walitangamana na mgonjwa huyo kabla ya kudhibitishwa kuwa na virusi hivyo.

Wambusi aidha amesema idara ya afya imeifunga zahanati hiyo ili kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya Korona.

Edward Nabangi Tale alipimwa na kupaikana na virusi vya korona alipofikishwa katika hospitali ya Life Care zaidi ya wiki moja iliyopita na kufariki dunia mapema hio jana.
Aidha jumla ya watu Nane katika familia ya mwendazake wamewekwa karantini.

Ripoti ya HILLARY KARUNGANI

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE