Huku shule zikiwa zimefunguliwa kote nchini, wazazi wa shule ya msingi ya Alomodoi kaunti ndogo ya Teso kusini kaunti ya Busia wameandaa maandamano wakilalamikia matokeo duni na ukosefu wa miundo msingi ya shule hiyo wakitaka mwalimu mkuu Patrick Omanyo Opilit na naibu wake kupewa uhamisho.
Wakizungumza na wanahabari mapema shuleni humo, Wazazi hao ambao waliwafungia nje walimu, wamelalamikia shule hiyo kuendelea kurekodi matokeo duni chini ya uongozi wa mwalimu mkuu Patrick Opilit.
Swala la ulevi katika kijiji hicho likichangia wengi wa walimu wa shule hiyo kushindwa kuwajibikia mafunzo kwa wanafunzi mbali na idadi kubwa ya walimu wakike kupewa likizo ya ujauzito swala wanalohoji imeathiri elimu ya wanao.
Wasimamizi wa usalama eneo hilo wakiongozwa na chifu Denis Opemi hata hivyo wameahidi kutafuta suluhu ya haraka.
By Hillary Karungani