Wito umetolewa kwa wakaazi wa Imakhaya – Sigalagala kwenye wadi ya Isukha Kusini eneobunge la Shinyalu kuendea chanjo ya virusi vya Corona.
Ni kauli yake Naibu chifu Wa Kata ndogo ya Shitochi Bi. Mildred Shihafu akihutubu kwenye mazishi yake Aaron Namsende maeneo ya Imakhaya ,huku akiwataka wenyeji kutoogopa kupata chanjo.
Aidha swala la Elimu amelipa kipaumbele akiwataka wazazi kupeleka wanao kwenye Taasisi za Kiufundi ikiwemo Chuo Anuwai cha kitaifa cha Sigalagala.
Bi Mildred amewataka wale ambao wamepoteza vitambulisho vyao vya kitaifa kupiga ripoti kwa kituo cha polisi kama njia mojawapo ya kujikinga na vitambulisho vyao kutumiwa kwa njia ya ualifu.
walio na mazoea ya kuvalia mavazi yanayowasitiri na nguo fupi hasa wasichana Naibu chifu huyo amesema kwamba NI wakati kwao kuzingatia Hilo au akabiliane nao inavyohitajika.
By Kennedy Babangida