Wazazi wametakiwa kuwapeleka wanao shuleni huku shule zikifumguliwa muhula wa kwanza baada ya likizo ya juma moja kote nchini

Ni kauli ya Donald Khavuchi chifu wa lokesheni ya Shisele kwenye eneo bunge la Ikolomani kaunti ya Kakamega akiwahutubia waombolezaji kwenye ibaada ya maombi na mazishi ya mama Henrieta Musina Inyanza katika kijiji cha Shirandala, lokesheni ndogo ya Mukongolo lokesheni ya Isulu eneo bunge la Ikolomani kaunti ya Kakamega 

Aidha amewarai wakenya kuzingatia sheria za kudhibiti msambao wa virusi vya corona ili kujiepusha na maafa zaidi yatokanayo na virusi hivyo

Kwa upande wake naibu chifu wa Lokesheni ndogo ya Mukongolo Andrew Shiveka akiwahimiza wakaazi kuwapeleka wanafunzi wote shuleni akiwaonya wazazi watakaogaidi amri hiyo kuwachukulia sheria kali huku akiwarai wale waliokamilisha kidato cha nne na kutofanikiwa vyema akiwashauri kujiunga na chuo cha kiufundi cha Bushiangala ili kujifunzia kozi mbalimbali 

Hali kadhalika amewatahadharisha wakaazi dhidi ya kutotumia vyema mto wa Mukongolo na kuwarusu watoto kuchezea akisema serikali itashughulikia mto huo hivi karibuni

Hata hivyo Shiveka amewashauri wakaazi pia kujitokeza na kuchukua kadi zao za huduma kwa wale ambao hawajapokea ilihali wamepokea ujumbe wa kudhibitisha kadi zao zimetolewa akiwataka kufika afisini mwake 

Wakati uo huo mwakilishi wadi mteule Ann Malekho akisema kuna mazungumzo ya kumshawishi mbunge wa ikolomani bernard shinali kusaidia shule ya shirandala kwa hali ya miundo msingi huku akiwarai wakaazi kumuunga mkono kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu ujao katika wadi ya Idakho ya kati kwa sasa ikiongozwa na mwakilishi wadi Charles Imbali

Huku wazee wa mtaa eneo hilo wakitilia mkazo swala la wazazi kuwapeleka wanao shuleni, na kumulika swala la mto wa mukongolo na swala la wizi hasa wakati huu wa mavuno ya mahindi

Ni hafla iliyoongozwa na kanisa katoliki la Musoli linaloongozwa na baba paroko Stanslaus Wabuti aliyewasilisha risala za rambirambi kutoka kwa viongozi wengine wa kanisa hilo

By Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE