Kiranja wa bunge la kitaifa ambaye pia ni mbunge wa Navakholo Emmanuel Wangwe ametaka ripoti ya sukari  iliyotolewa na jopo lililoongozwa na gavana wa Kakamega  na aliyekuwa waziri wa kilimo Mwangi Kiunjuri na gavana wa Kakamega Wycliffe  kuwasilishwa bungeni ili iidhinishwe na rais Uhuru Kenyatta ili ianze kutekelezwa kuokoa wakulima wa miwa.

Akizungumza kwenye hafla ya elimu katika shule ya msingi ya Namirama ene bunge lake la Navakholo Wangwe amesema kuwa kwa sasa wazazi wengi waliokuwa wakitegemea miwa wameshindwa kulipia wanao karo ya shule na kumtaka gavana Oparanya kuona kuwa ripoti hiyo inaidhinishwa jinsi vile ripoti za sekta zingine za kilimo zilitekelezwa.

Wakati huo uo Wangwe amemtaka rais Uhuru Kenyatta kufanya haraka kuweka mwekezaji wa kufufua kiwanda cha sukari cha Mumias  huku  akiwataka wenyeji wa kaunti ya Kakamega kuunga mkono mwekezaji yeyote atakayepewa  majukumu ya kufufua kiwanda  hicho kama njia  moja ya kuzuia unyanyapa unaofanyiwa wakulima na kampuni za kibinafsi.

Kwa upande wa elimu Wangwe ameunga mkono agizo la waziri wa elimu Profesa George Magoha la kupiga maarufuku siasa kwenye mashule akisema kuwa siasa shuleni zinachangia pakubwa matokeo mabaya.

By Sajiida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE