Seneta mteule katika kaunti ya Kakamega Naomi Shiyonga amewataka wazazi kuwalinda vyema wanao wanapo rejea nyumbani katika likizo ili wasijihusishe na visa vya utovu wa nidhamu miongoni mwao

Akiwahutubia waombolezaji kwenye hafla ya mazishi katika kijiji cha Shamoni eneo bunge la Malava seneta Shiyonga amewahimiza wazazi kuhakikisha wanao wanaishi maisha mema huku akiwashauri kuwahusisha na kazi shambani kama njia moja wapo ya kuwaepusha na visa potovu.

“tafadhali watoto wanarudi nyumbani acha tulinde watoto wetu. Tukae na watoto wetu tuwafunze kulima tuwafunze biashara maana nawakuja likizo na msimu wa kupanda acha watoto wajue kufanya kazi na waelewe jinsi wazazi wanapata chakula na pia karo yao ya shule alisema shiyonga.”

Kauli ya seneta Shiyonga imepigwa jeki na mwenyekiti wa chama cha walimu KNUT tawi la Malava ambaye pia ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Shamoni Simon Ondeyo.

Naye mtawala wa eneo hilo Vitalis Otisa ambaye pia aluhudhuria mazishi hayo amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wale watakaopatikana wakijihusisha na densi za usiku maarufu kama disco matanga.

“tumekataza disko matanga na pia watoto kwenda matanga usiku. Na wazazi tafadhali usiseme mtoto amekushinda, mtoto umezaa atakushinda namna gani wazazi tujukumike kuwalinda watoto wetu na tuwaelekeze kwa maadili mema vilevile tuwapeleke watoto shuleni  wasikae nyumbani.” Alisema mtawala

Story by Lihavi Imelda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE