Huku shughuli za masomo zikirejea nchini wiki hii, onyo limetolewa kwa wazazi ambao wanao walipachikwa mimba wakati walikuwa nyumbani dhidi ya kuwaficha na kuwazuia kurudi shuleni.

Haya ni kwa mujibu wa afisa wa afya katika eneo bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega Lonah Omumia akizungumza katika hafla ya kuhamasisha jamii dhidi ya mimba za mapema ambapo amesema serikali imewaruhusu wanafunzi hao kurudi shuleni na itakuwaa vyema wao kuendeleza masomo yao.

Ni kauli iliyoungwa mkono na msimamizi wa maswala ya uzazi na dhuluma za kijinsia katika eneo bunge hilo Esther Mboya.

Wawili hao aidha wamewakashifu vikali wanaodhulumu watoto wa kike na wakiume kimapenzi huku akiitaka jamii kushirikiana nao ili kupigana na dhuluma hizo.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE