Baraza la wazee kaunti ndogo ya Khwisero kaunti ya Kakamega wamezindua mchakato wa kuwaleta pamoja wawakilishi wadi na mbunge Christopher Aseka wakisema tofauti miongoni mwa viongozi hao zimekwamisha maendeleo
Wakiongozwa na mwenyekiti … wamesema hawaridhishwi na vita vya maneno vinavyoshuhudiwa kutokana na wawakilishi wadi wote wanne kuwa na mrengo wao huku mbunge akisalia na mrengo wake
Wazee hawa wanasema tofauti za viongozi zimeathiri miradi ambayo ingewafaidi hasa maswala ya afya ambayo yanawaathiri wakongwe mara kwa mara, na nia ya ujenzi wa kituo cha tamaduni ambao unapaswa kufanikishwa na juhudi za pamoja za viongozi