Waziri wa biashara katika serikali ya kaunti ya Kakamega Robert Makhanu amewataka akina mama kutumia nafasi ya fedha za serikali kujiendeleza kiuchumi
Akiwahutubia wanachama wa makundi ya akina mama eneo la Butere, Makhanu amesema serikali ya kaunti imetenga raslimali nyingi za kuwasaidia wananchi hasa akina mama na amewataka kushirikiana na maafisa wa serikali nyanjani kupata miradi hiyo
Ni kako kilichoandaliwa na kikundi cha akina mama cha Waridi na kupitia kwa kiongozi wao Rechael Mukuna wameisuta serikali kwa kukosa kuandaa manthari mwafaka katika masoko hasa kwa akina mama
Wanaitaka serikali kuandaa vikao mashinani mara kwa mara na wananchi kuwapa ufahamu wa sharia na mipangilio
Story by James Boaz Shitemi