Washukiwa wanne wa wizi wa  kimabavu wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kabras  baada ya kukamatwa na maafisa wa polisi wakiwa na vifaa vingi vya elektroniki vinavyodaiwa kupotea sehemu nyingi za eneo la Malava. 

Akizungumza na wanahabari mjini Malava kamanda wa polisi eneo la Kabras Peter Mwanzo amedokeza kuwa washukiwa hao ni miongoni mwa genge la wezi ambalo limekuwa likiwahangaisha wakazi wa eneo la Magharibi akihoji kuwa wanne hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria.

Kamanda huyo amefichua kuwa kulingana na uchunguzi uliyofanywa na maafisa wa polisi ni kuwa genge hilo linaendeshwa na washukiwa sugu ambao huenda wanaendesha biashara ya kuuza vifa vya elektroniki na huwasaidia wanapokuwa na kesi mahakamani.

Aidha kamanda huyo ameonekana kuzilaumu mahakama za humu nchini kwa kile anadai zinahujumu utendakazi wa maafisa wa polisi kwa madai ya kuwaachilia huru washukiwa husika.

Ametumia fursa hiyo kuwataka waathiriwa wa wizi huo kujiwazilisha mbele ya polisi na stakabadhi muhimu ili warejeshewe mali yao.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE