Washukiwa wawili wa wizi wameuwawa na wakazi wenye hamaki usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Eshikangu, kata ya Lunza eneo bunge la Butere kaunti ya Kakamega baada ya kufumaniwa wakisafirisha nguruwe anayedaiwa kuwa wa wizi.

Inadaiwa kuwa wawili hao ambao walipatikana kwa boma la mwenyeji mmoja mwendo wa saa tisa usiku wakiwa wamembeba nguruwe kwa pikipiki na mwenyeji huyo alipopiga mayowe wenyeji wenye hamaki walifika kwa haraka na kuwafumania kisa wakawachoma pamoja na pikiki waliokuwa nayo.

Wenyeji hao wamelalamikia ongezeko la wizi wa mifugo eneo ni kwani magari huzuru eneo hili majira ya usiku yakitumika kusafirisha mifugo.

Mzee wa mtaa huu joseph ameyo amesema kuwa visa vya wizi wa mifugo vimeongezeka sana eneo hili na kutoa wito kwa wenyeji kuacha kujichukulia sheria mikononi. Miili ya wawili hao inahifadhiwa katika chumba cha wafu cha St.Marys Mumias

By  Kefa Linda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE