Wito unazidi kutolewa kwa jamii ya mulembe kuwa imara na kukipigia debe chama cha ANC na kumuunga mkono kinara wa chama hicho Musalia Mudavadi kwenye azma wa kutwaa uongozi wa nchi hii kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka wa 2022
Wakihutubu kwenye mazishi ya mama Emily Angatia mkewe aliyekuwa waziri wa afya katika serikali ya Moi pia mbunge wa Malava Joshua Angatia mbunge wa eneo hilo Moses Malulu Injendi, mwakilishi wadi wa Kabaras Magharibi David Ndakwa na Caleb Sunguti wamesema kuwa wakati umewadia wa kila kiongozi wa kutoka eneo hilo kumpigia debe Mudavadi kupata uongozi wa nchi ya Kenye wakiapa kusimama naye hadi mwisho
Nao wanachama wa chama cha KANU ambacho marehemu Angatia alikuwemo wakiongozwa na Daniel Jirongo walipeana rambirambi zao huku wakisisitiza kuwa hawatatingizwa na wenye wanaungana kwa ANC na kusema kuwa watafuata mwelekeo wa kinara wao Gideo Moi.
By Richard Milimu