Genge la watu wanne waliyojihami kwa bunduki walimteka nyara mwanamme mwenye umri wa miaka 63 na kutoweka na takribani shilingi elfu mia saba pesa taslimu alizotoa kwenye benki moja mjini Kakamega.

Kulingana na mzee Alphonce Maina amehoji hiki kuwa wanne hao waliyokuwa wamejihami walimfuata hadi nyumbani kwake katika kijiji cha Handidi na kumuamuru aingie gari ndogo aina ya saloon ambapo aliachwa katika kijiji cha Tande huku wakifanikiwa kutoweka na shilingi elfu mia saba pesa taslimu.

“Nilienda kwa bank kuchukua pesa bank teller akaniambia nirudi nilete agreements za shamba nilipo leta alithibitisha na nikamwambia natoa shilingi elfu miasaba, akaniesabia pesa akanipea na akaniambia nitoe mask anataka kuniona vizuri, nilipotoka kwa bank nikienda nyumbani kufika karibu na gate, gari ndogo ya green ilinipita na ikaingia kwa compound yangu na wakatoa pingu, over over na bunduki wakaanza kuniita mwizi na wakaniforce kuingia kwa gari na wakapiga bibi yangu teke akaanguka chini na wakatoa gari mbio.” alieleza mzee

Mzee maina amefichua kuwa wanne hao walimfunga kwa pingu na hata walimtishia kumuua endapo angepiga mayowe.

“Walienda na mimi wakaniambia nikipiga kelele wataniuwa nilifikishwa tande na wakanitoa kwa gari kuangalia number plate walikua wameifunga na gazeti.”

Ni kisa kilichoshudiwa na mkazi mmoja wa Malava ambaye pia ni mhudumu wa bodaboda katika eneo la Tande.

Niliona gari ikiingia njia ya tande na ilikua imefunikwa number plate na gazeti na walitoa mzee ndani na wakamrusha nnche na ikatota ikaelekea upande wa webuye.”

Hata hivyo tayari maafisa wa upelelezi kutoka eneo bunge la Malava wameanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE