Kulingana na utafiti uliofanywa na wizara ya afya kaunti ya Kakamega imebainika zaidi ya wasichana 6,000 wa umri wa chini ya miaka 18 walipachikwa mimba  za mapema, huku wengi wao wakipoteza uhai wao kupitia uavyaji mimba kwa njia isiyo salama.

Hii ni kwa mujibu wa afisa anayesimamia hospitali kuu ya Navakholo kwenye Warsha iliyoandaliwa eneo bunge la Navakholo na shirika la IPAS linaloshughulikia maswala ya uavyaji wa mimba kwa njia salama.

Huku naibu kamishna wa wa eneo la Navakholo Joshwa Mutisywa akitoa onyo kali kwa wazee wanyumba kumi na wazee wa mitaa kwa kudaiwa kujihusisha na mahakama za kangaroo  kati ya wale wanaojihusisha na kuwadunga mimba za mapema watoto wa shule.

Naye afisa wa kundi la Bumulusi linaloshughulikia dhuluma za kijinzia bi.Pamela Wambongo, akisema wengi wa wasichana wamepoteza uhai wao kupitia mikononi mwa madaktari gushi wakati wa kuavya mimba.

By Linda Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE