Wakazi wa eneo la Kwang’amor wadi ya Amukura ya mashariki kaunti ndogo ya Teso kusini kaunti ya Busia wameandaa maandamano ya amani kumkashifu mwakilishi wa wadi hiyo Moses Echopat kufuatia hatua yake ya kupuuza Barabara za eneo hilo.

Wakiongozwa na Dismas Omukaga wenyeji hao wakiwemo wahudmu wa Bodaboda wanasema wanapitia hali ngumu ya usafiri kutokana na hali duni ya Barabara za eneo hilo huku mwakilishi huyo akidaiwa kulifumbia jicho  tatizo hilo.

Wakizungumza na kituo hiki katika Soko la Kwang’amor, wanasema shughuli za masomo na kilimo pia zimeathirika pakubwa kutokana na hali mbovu ya Barabara za eneo hilo.

‘Aidha wanasema magonjwa yanayotokana na maji machafu pia yanawakodolea macho.

Wameapa kuandamana zaidi na kupanda migomba kumshinikiza mwakilishi huyo kuwatengenezea Barabara hizo kwa kutumia fedha za hazina ya maendeleo ya wadi.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE