Wazazi kukosa kuwajibikia majukumu yao pamoja na umaskini vimetajwa kama vyanzo vya mimba za mapema miongoni mwa watoto wa kike katika jamii

Haya ni kulingana na mkewe mbunge wa Lurambi Titus Khamala bi Roselyne Khamala

Bi Khamala amedokeza kuwa anafanya kila wawezalo kuhamasisha uma kuhusu athari za mimba hizo

Amewatahadharisha wazazi dhidi ya kuwaruhusu watoto chini ya umri wa miaka 18 kupanga uzazi akisema kuwa hili ni hatari kwa afya za watoto hao mbali na kuchangia kuenea kwa magonjwa ya zinaa

Kauli hiyo iliungwa mkono na kamishana wa kaunti ndogo ya Cheptais Samwel Towet aliyesema kuwa anashirikiana na vyongozi wenza wa utawala kuhamasisha jamii eneo hilo kuhusu swala la mimba za mapema

Kwa upande wake mkurugenzi wa elimu kaunti ndogo ya Cheptais Eric Were amehoji kuwa mimba za mapema miongoni mwa watoto wa kike huathiri pakubwa viwango vya masomo eneo hilo

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE