Wakaazi wa Teso kaunti ya Busia wametakiwa kukumbatia mradi wa bwawa la Ang’ololo unaotarajiwa kujengwa eneo hilo kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
Mkurugenzi wa idara ya maji kaunti ya Busia James Imwene amesema kuwa mradi huo utawanufaisha wakaazi wa Busia na hata wa nchi jirani ya Uganda
Kwa upende wake mwakilishiwadi ya Amurai Kaskazini ambaye pia ni naibu spika wa bunge la kaunti ya Busia okale Murunga amewataka wakaazi kuhusika kwenye vikao vya maoni kuhusu jinsi utakavyojengwa mradi huo na namna watakavyonufaika
By James Nadwa