Zaidi ya wakaazi 15,000 kutoka kata ya Khalwenge Endebes kaunti ya Transnzoia wako kwenye hatari ya kupoteza mashamba yao kwa kukosa hatimiliki
Wakaazi hao sasa wanaitaka serikali kuharakisha mpango wa kutoa hatimiliki kwani baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa matapeli wanatishia kuwapokonya mashamba hayo wakitumia kisingizio cha wakaazi kukosa stakabadhi za kumiliki mashamba hayo
Kauli hiyo iliungwa mkono na kiongozi wa kundi la wakaazi wasio na ardhi kutoka timboroa la Timboroa Squaters kaunti ya Transnzoia Moses Masinde aliyetaka zoezi la kuwapa mashamba masquota wa shamba la Chepchoina kuharakishwa
By James Nadwa