Mashirika mbalimbali ya kijamii ya Bonde la Ufa sasa yanamtaka rais kuchukua hatua ya dharura kukabili machafuko yalosababishwa na wezi wa mifugo eneo la Ol Moral Laikipiya
Kwenye kikao na wanahabari mjini Kitale mwenyekiti wa mashirika hayo Kefa Were amesikitikia matamshi ya hivi maajuzi ya mshirikishi wa utawala eneo la Rift Valley George Natembeya kuwa wezi hao wa mifugo wamejihami kuliko vikosi vya serikali
Ameyataja matamshi hayo kuwa kejeli kwa vitengo vya usalama wa nchi haswa tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu ujao
By James Nadwa