Maswala ya ukosefu wa usalama na utumiaji wa mihadarati imekidhiri katika kaunti ya Uasin Gishu hasaa katika eneo la Langas.

Hii leo county kamishina wa eneo la Uasin Gishu Stephen Kihara amekua na kikao na wakaazi wa Langas wakijadili njia mbandala  za kukabiliana na utumizi wa dawa za kulevya na uhalifu katika eneo Hilo.

Kamishina huyo amesema kuwa janga la korona limekua kizingiti kikuu kwa Askari kutekeleza majukumu yao Kama kawaida kwani ratiba yao iliadhirika kwa kiwango kikubwa.

Dan Mwangi ambaye ni mwanabiashara na mkaazi wa eneo Hilo amesema kuwa wasimamizi wa nyumba kumi wazee wa mtaa na machifu wamekosa ulinzi wa kutosha hii ikifanya maisha yao kua hatarini baada ya chifu wa eneo Hilo kuvamiwa na kuumizwa.

Mkaazi wa langas Eve Adongo amewatetea wazee wa mitaa na machifu kwani wanafanya kazi nzuri na kuwaelekezea kidole Cha lawama polisi kwa utepetevu wao na kuchukua hongo mkazi huyo pia amesema kuwa watachukua hatua mikononi mwao na kuwakamata askari watakaokua wakichukua mlungula.

By Sharon Lukorito

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE