Vijana katika kaunti ya Kwale wamehimizwa kukumbatia masomo ya kiufundi ili waweze kupata ujuzi wa kuwapa kazi.

Mkurugenzi wa masuala ya vijana katika kaunty hiyo Kent Simiyu, amesema kozi zinazotolewa katika taasisi za kiufundi katika kaunti hiyo, zinahitajika katika soko la ajira kwa sababu zinawawezesha wanafunzi kujiajiri wenyewe.

Alitoa wito wa kubadilishwa kwa mawazo kuhusu taasisi za kiufundi na akawataka vijana wafanye kozi za kiufundi ili kuweza kutekeleza ajenda nne kuu za maendeleo.

Simiyu alikariri kwamba kwa wakati huu, eneo la pwani linakumbwa na uhaba mkubwa wa mafundi kama vile wa mifereji ya maji, maseremala, wachomeleaji vyuma na maseremala miongoni mwa ujuzi mwingine.

Aliongeza kusema kwamba mpango wa kuwaajiri vijana humu nchini, unaimarisha hali ya maisha ya vijana wa nchi hii kupitia kwa mafunzo ya kiufundi.

Hadi kufikia sasa mpango huo wa kuwaajiri vijana,umetoa mafunzo kwa vijana elfu tano katika kaunti ya kwale huku vijana 1,600 wakipokea ruzuku za shillingi 40,000 za kuanzisha miradi ya kujipatia mapato.

By Lihavi Imelda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE