Mjumbe wa Bumula kwenye bunge la taifa  Mwambu Mabonga amesikitikia kile alichokiita kama vijana kutumika vibaya  haswaa wakati wa uchaguzi.

Mjumbe huyo amesema kuwa vijana wengi hukubali kuhongwa hela kidogo ili kuzua vurugu katika hafla za matanga na hadhara zinginezo hivyo basi kuwataka vijana kuwapuzilia mbali wanasiasa wanaowatenganisha kwa misingi ya kikabila.

Mabonga aidha ametumia fursa hiyo kuwaonya vijana kutumia mitandao ya kijamii vibaya huku akiwarai kujiepusha kusambaza jumbe za chuki ili kuinusuru nchi dhiti ya kutumbukia kwenye mizozo ya kisiasa.

Mwambu aidha amemsihi rais Uhuru Kenyatta na naibu wake Dkt William Samoei Ruto kuweka kando tofauti zao za kisiasa ili kuwahudumia wakenya

Ameyasema hayo kwenye ujumbe alioutuma kwa wanahabari mjini Bungoma.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE