Afisa mkuu wa elimu kaunti ya Vihiga Hellen Nyang’au amewatahadharisha wazazi eneo hilo watakaokosa kuwapeleka wanao shuleni kuwa watachukuliwa hatua za kisheria
Bi Nyang’au amesema kuwa serukali kaunti hiyo Inafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa watoto wote haswa walokalia mtihani wa darasa lq nane wanaojiunga na kidato cha kwanza
Amewataka wazazi kutochukulia ukosefu wa karo kama kisingizio cha kutowapeleka watoto wao shuleni akisema kiluwa serikali imejitolea kugaramia masomo ya wanafunzi katika shule zote za upili humu nchini
By James Nadwa