Wakulima wa maziwa kutoka mtaa wa Bukura eneobunge la Butere wanalalamikia ushindani kutoka kwa serikali ya Kakamega kwenye biashara hiyo
Wakiongea na idhaa hii vyongozi pamoja na wanachama wa shirika la Butsotso South Dairy Cooperative wakiongozwa na Joel Khaweri wanasema kuwa kituo cha serikali ya kaunti ya Kakamega cha Bukura Agri Smart farm kimekuwa tishio kwa kilimo chao
Wanasema kuwa hii ni kutokana na ushindani mkali wanaopata kutoka kwa kituo hicho
Wanasema kuwa imekuwa vigumu kwa wakulima kutoka eneo hilo kushirikiana na kituo hicho cha serikali
Wameeleza manufaa ya shirika lao haswa kwa wakulima wadogo kutoka eneo hilo tangia lilipozinduliwa
By James Nadwa