Hali ya huzuni na hofu imetanda katika chuo kikuu cha Masinde Muliro(MMUST) kaunti ya Kakamega baada ya mwanafunzi mmoja wa kike kupatikana akiwa ameuliwa kinyama.


Macline Achieng ambaye hadi mauti yake alikuwa mwanafunzi wa shahada ya elimu,mwili wake ulipatikana asubuhi ya kuamkia Jumatano ukiwa nusu uchi na majeraha katika sehemu mbalimbali za mwili.

Maafisa wa polisi wameanza upelelezi wao kubaini yaliyotokea huku ikituhumiwa kuwa huenda mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatu alibakwa kabla ya kuuliwa kwani sehemu zake za siri zilikuwa na matone ya damu.


Wataalam wa kuchunguza mauaji wanafanya uchunguzi wao kubaini nini haswa kilichosababisha mauti hayo huku ikituhumiwa kuwa huenda alipoteza damu baada ya kugongwa kwenye kisogo na kifaa butu.


Inashukiwa kuwa huenda marehemu aliuliwa ndani ya nyumba yake ya kukodishwa iliyo katika eneo la Kenfinco mjini Kakamega kabla ya mwili kubebwa na kutupwa mita kadhaa kutoka nyumba hiyo kwani kulikuwa na athari za damu kutoka kwa nyumba kuelekea kwa ngazi za ploti hiyo.


“Ni kama walikuwa na aliyemtendea unyama huo kwa nyumba ama alidanganywa kufungua mlango kwani hakukuwa na ishara yoyote ya kuvunjwa kwa mlango huo na pia haikuonekana kana kwamba kuna chochote kilichokuwa kimeibiwa. Hata hivyo tuliweza kuona matone ya damu ndani ya nyumba hiyo” Ronnie alisema


Wanafunzi waliogahdabika kutokana na kuuliwa kwa mmoja wao waliandamana wakilalamikia ukosefu wa usalama kabla ya kutawanywa na maafisa wa polisi.


Mkutano wa seneti ulifanyika siku ya Jumatano ulipendekeza hatua kadhaa za kulinda usalama wa wanafunzi zikiwemo kuwekwa kwa mataa katika maeneo yaliyoathirika, kujengwa kwa kituo cha polisi katika maeneo ya Kefinco na Juakali, kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa wanafunzi na mengineo.


Muungano wa wanafunzi wa chuo hicho, MMUSO, umeagiza wanafunzi wanaoishi pande za Kefinco kuhama na kuwasihi kutembea kwa makundi haswa masaa ya usiku.
By marseline musweda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE