Wafanyibiashara kutoka maeneo mbali mbali wameombwa kukumbatia zoezi la chanjo kama njia mojawapo ya kujikinga na kudhibiti msambao wa ugojwa wa covid 19
Akizungumuza moja kwa moja na kituo hiki Sammy Mmoja amewahimiza wafanyibiashara wenza kuendea chanjo hiyo muhimu
Mimi nawahimiza wafanyibiashara wenzangu tuende tupate chanjo hii ya corona. Haichukui muda mrefu. Msifate propaganda za watu kuhusiana na chanjo hii ya corona. Mimi binafsi nimedungwa na sijakua na madhara yoyote
Vile vile amezungumzia kufifia kwa biashara na kuwahimiza wateja kutembelea banda lake kwa minajili ya kupata bidhaa zote za urembo ambazo wanazihitaji kwa bei nafuu
By Samson Nyongesa
