Timu ya vijana wa West Kenya All-Stars waliandikisha alama tatu kwenye ligi ya FKF tawi la kaunti ya Kakamega kwa kuilambisha mahasimu wao undugu kutoka eneo jirani la Navakholo bao moja mtungi.

Mechi hiyo ilisakatwa katika uwanja wa Shamberere eneo bunge la Malava huku Renson Seth akaifungia timu yake ya West Kenya mnamo dakika ya thelathini na nane kipindi cha kwanza japo vijana wa undugu walitawala uwanja kipindi hivho  chote bila kuona lango la wapinzani.

Akizungumza na kituo hiki kocha wa West Kenya All-Stars Wycliffe Waswani alifurahia ushindi huo na pia kuwavulia kofia wapinzani wao kwa kuonyesha mchezo wa kusisimua.

Kwa upande wake kocha wa undugu Kevin Wasike alikubali kichapo hicho cha bao moja ili akakosoa usimamizi wa mechi hiyo kuwa sababu kubwa ya kushindwa kwao.

Kwenye mechi nyingine ya ligi hiyo timu ya Sleemaz ikatoka sare ya bao moja dhidi ya Kabras United, Lugusi ikalemea Mayoni magoli 4 kwa 2 nayo Kingdom ikiandikisha ushindi wa bao moja kwa nunge dhidi ya Homebyz.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE