Huku Rais Uhuru Kenyatta akitarajiwa kuongoza taifa kuadhimisha siku kuu ya Madaraka jijini Kisumu, wito umetolewa kwake kuangazia swala la kufufua viwanda vya sukari eneo la Magharibi kwa manufaa ya wakulima.

Haya ni kwa mujibu wa  mbunge wa Kabuchai Majimbo Kalasinga anayehoji kuwa eneo hili linategemea pakubwa kampuni hizo, akisema zinastahili kurejelea hali yao ya kawaida  akisema kila mwananchi anastahili kufurahia huduma za serikali.

Wakati uo huo majimbo amewataka wananchi kuheshimu uamuzi wa mahakama baada ya majaji wa mahakama kuu kuharamisha mchakato wa kuifanyia marekebisho katiba kupitia mfumo wa BBI.

Aidha mbunge huyo amedokeza kuwa tayari  wamekamilisha kupiga msasa wanafunzi watakaonufaika na ufadhili wa fedha za basari.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE