Maafisa wa polisi kutoka eneo bunge la Ikolomani kaunti ya Kakamega wanachunguza kisa ambapo mwili wa mtoto wa kike wa miaka mitano umepatikana ukiozea ndani ya choo katika kijiji cha Imalaba kata ndogo ya Shabwali.

Kulingana na wenyeji wa kijiji hicho, mtoto huyo alitoweka tarehe 17 mwezi huu kabla ya mwili wake kupatikana hii leo katika boma ya jirani, kutokana na uvundo mkali uliokuwa ukitoka chooni humo.

OCPD wa Ikolomani Joseph Chesire amethibitisha kisa hicho na kusema mwili huo tayari umechukuliwa na kupelekwa katika hifadhi ya wafu ya hospitali kuu ya Kakamega ambako utafanyiwa upasuaji ili kubaini chanzo cha mauti hayo.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE