Mwakilishi wadi ya Endebess ambaye pia ni kiongozi wa wengi katika bunge la Kaunti ya Trans-Nzoia Parick Kisiero ametoa wito kwa Mshirikishi wa Bonde la ufa George  Natembea  kupitia kwa wizara ya usalama wa ndani kuajiri Maskaunti  ilikuimarisha doroa katika msitu na mbuga ya Wanyama ya Mlima Elgon.

Akihutubu eneo la Endebess Kisiero amesema kupitia kwa maskaunti hao  kwa ushirikano na maafisa wa usalama eneo hilo watasadia kukabili ukosefu wa usalama,Ulaguzi wa silaha ndogo ndogo maeneo ya mipakani pamoja  na uwindaji haramu.

Aidha Kisiero amemtaka  Bwana Natembea kubuni divisheni nyingine 4  eneo bunge hilo mbali na kata ndogo kahdaa kama nji moja wapo ya kuimarisha  uwakilshi wa utawala katika eneo bunge hilo ambalo kwa sasa inaupungufu wa uwakilishi wa utawala.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE