Kulishudiwa kizaazaa katika kituo cha matatu cha Kakamega baada ya joka nyeusi la urefu wa futi tano lilokuwa lisafirisha na abiria ndani ya matatu kudondoka na kukanyagwa na gari lilokuwa likitoka na upande wa nyuma.
Kulingana na walioshuhudia joka hilo lenye rangi nyeusi na rangi nyeupe shingoni lilidondoka kutoka kenye mtungi uliokuwa ukisafirishwa kutoaka maeneo ya eldoret kuelekea mjini Kakamega.
Inadaiwa huenda joka hilo lilizidiwa na harufu ya mafuta ya petroli na wakati gari hilo lilofika kwenye kituo hichocha magari likapata nafasi ya kujinasua kutoka kwe nye harufu ya mafuta ambapo liliganyagwa na gari lilokuwa likitoka na upande wa nyuma.
Tumeona maajabu leo yani mtu amebeba nyoka kwa gari kutoka Eldoret hadi hapa Kakamega. Ni kama arufu ya petrol iliilemea ndo maana ikatoka nnje ya mtungi na imekanyagwa na gari ambalo lilikua limetokea nyuma ya gari hiyo nyoka ilikua ndani. Hii nyoka imekua ya black na white na ni kubwa. Hii ni kama uchawi mi sijawai ona maneno kama haya.