Katibu wa kudumu katika idara ya elimu ya juu na utafiti balozi Simon Nabukwesi ameongoza hafla ya upanzi wa miti katika shule ya upili ya wavulana ya Cheptais eneobunge la Mlima Elgon huku wito ukitolewa kwa wananchi kupanda miti kwa wingi ili kutunza mazingira hasa kwenye msitu wa Cheptais ambao ulikuwa umeharibiwa pakubwa.

Akihutubu baada ya kuongoza hafla hiyo ya upanzi wa miti Nabukwesi amesema hatua ya upanzi wa miti kwenye msitu wa Cheptais iliafikiwa baada ya kubainika kuwa asilimia kubwa ya msitu huo ilikuwa imeharibiwa na shuguuli za kilimo, huku akiwataka wananchi kuboresha mazingira ili kuzuia momonyoko wa ardhi ambao umekuwa ukishuhudiwa kila kuchao.

Aidha Nabukwesi amewapongeza washikadau kutoka sekta mbalimbali kwa kuhakikisha hafla hiyo inaendeshwa kwenye shule ambapo miche elfu moja ilipandwa kwenye shule hiyo na kuwataka wananfunzi kuwa msitari wa mbele kupanda kisha kutunza miti hiyo.

Naye afisa wa mazingira kaunti ya Bungoma Vitallis Osodo akidokeza kuwa watazidi kuwahusisha wananchi kwenye hafla hizo ili kuhifadhi msitu wa Cheptais.

Tutaendelea kupanda miti na tuhusishe kila moja kwa upanzi huo wa miti katika msitu wetu wa Cheptais ambao umeharibiwa pakubwa. kila mmoja atahusika kwa upanzi wa miti na kutunza huu msitu hatutapanda miti kwa msitu pekee bali miti tutazipanda kila eneo la Mlima Elgon Alisema afisa wa mazingira kaunti ya Bungoma  

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Wycliffe Nyongesa Waliaula akipongeza shuguuli  hiyo huku akifurahia matokeo bora ya mtihani wa kitaifa wa mwaka jana.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE