Ajali mbaya ya barabarani imetokea eneo la Horemo kwenye barabara kuu ya Kakamega-Webuye ikihusisha tuktuk na gari dogo aina ya Toyota.
Jotham Akala mmoja wa walioshuhudia ajali hii alisema kuwa tuktuk ilikuwa ikielekea mji wa Kakamega kwa mwendo wa kasi huku ikifwatwa na pikipiki kadhaa na hapo ndipo iligongana na gari lililokuwa linaelekea Malava.
Jotham amesema kuwa ndani ya tuktuk kulikuwa na mama ambaye alikuwa anapiga nduru huku akiomba usaidizi kwani alikuwa ameibiwa pesa zake jambo ambalo lilifanya dereva wa tuktuk kuruka kutoka ndani na kuelekea kwenye shamba la mahindi lililokuwa karibu
Nilisikia mwanamke akipiga nduru ndani ya tuktuk akiomba usaidizi kwamba ameibiwa pesa yake na kisha baadaye Tuktuk hiyo ikaweza kusababisha ajali kwa maanake dereva alikua amemwibia mama huyo fedha zake na pia baada ya kusababisha ajali hiyo aliweza kutorokea kwa mahindi ambayo iko hapa kando ya barabara
Naye Jeremiah Jeti mkaazi wa oremo ameitaka serikali kuweka matuta sehemu ya oremo ili kuzuia ajali za kila mara zinazofanyika mahali hapo
Tunaomba serikali mutuekee hapa matuta. watu wamekufia hapa wengi sana kupitia kwa ajali kwa hivyo tunaomba tu mueze kutuekea matuta hapa
By Mary Owano