Ajali   mbaya ya barabarani imetokea eneo la Horemo kwenye barabara kuu ya Kakamega-Webuye ikihusisha tuktuk na gari dogo aina ya Toyota.

Jotham Akala  mmoja wa  walioshuhudia ajali hii alisema kuwa tuktuk ilikuwa ikielekea  mji wa Kakamega kwa mwendo wa kasi huku ikifwatwa na pikipiki kadhaa  na hapo ndipo  iligongana na gari lililokuwa linaelekea  Malava.

Jotham amesema kuwa ndani ya tuktuk kulikuwa na mama  ambaye alikuwa anapiga nduru huku akiomba usaidizi kwani alikuwa  ameibiwa pesa zake  jambo ambalo lilifanya dereva wa tuktuk  kuruka kutoka ndani na kuelekea kwenye shamba la mahindi lililokuwa karibu

Nilisikia mwanamke akipiga nduru ndani ya tuktuk akiomba usaidizi kwamba ameibiwa pesa yake na kisha baadaye Tuktuk hiyo ikaweza kusababisha ajali kwa maanake dereva alikua amemwibia mama huyo fedha zake na pia baada ya kusababisha ajali hiyo aliweza kutorokea kwa mahindi ambayo iko hapa kando ya barabara

Naye Jeremiah Jeti mkaazi wa oremo ameitaka serikali kuweka matuta sehemu ya oremo ili kuzuia ajali za kila mara zinazofanyika  mahali hapo

Tunaomba serikali mutuekee hapa matuta. watu wamekufia hapa wengi sana kupitia kwa ajali kwa hivyo tunaomba tu mueze kutuekea matuta hapa

By Mary Owano

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE