Utengenezaji wa barabara za mashinani unaendelea licha ya changamoto za kifedha kuwepo kwenye kaunti.
Ni usemi wake mwakilishi wa wadi ya Butsotso Mashariki iliyo katika kaunti ndogo ya Luhambi kaunti ya Kakamega Matthews Nyangweso.
Akiwahutubia waombolezaji katika ibaada ya mazishi ya mwenda zake Isaac Muchanji katika kijiji cha Eshitoto, mwakilishi wadi huyo anawahimiza wakaazi kwamba ukarabati wa barabara katika wadi hiyo utakamilika hivi karibuni kwa kulimwa umbali wa kilomita ishirini na tano.
Kuhusu basari za shule kwa wanafunzi, vilevile anawahakikishia wazazi kuwa kabla ya shule kufunguliwa juma lijalo, mgao wa basari hizo utakuwa umewasilishwa katika kila shule.
Kwa upande mwingine anawarai wakaazi wa maeneo ya Eshitoto kuhusu mpango wa kuanzisha shule ya msingi maeneo hayo kwa kuendeleza shule ya chekechea iliyo katika maeneo hayo.
Anawaitisha wakaazi hao kufika kwenye kikao cha kulijadili swala hilo siku ya ijuma tarehe 23-7-2021 mwendo wa asubuhi saa tatu huku akiwaomba kuzingatia masharti ya covid-19.
Ni ibaada iliyosimamiwa na kanisa la Eshitoto PAG chini ya mchungaji Abel Ivelia
By Wycliffe Sajida