Wakaazi wa kaunti ya Pokot Magharibi wanaoishi maeneo ambayo hukubwa na mafuriko na mumomonyoko wa udongo wameanza kuhamia maeneo salama kwa kuhofia maisha yao baada ya mvua kubwa kunyesha katika sehemu hiyo.

Hii ni baada ya matukio ya mwaka 2019 na 2020 katika kaunti hiyo ambapo mafuriko na maporomoko ya ardhi yalisababisha vifo vya watu 60.

Kaunti ndogo ya Pokot kusini siku ya Alhamisi, sehemu kadhaa zilishuhudia maporomoko ya ardhi baada ya mvua kubwa kunyesha kwa saa kadhaa.

Fredrick Kimanga ambaye ni naibu kamishina wa kaunti ndogo ya Pokot Kusini, alithibitisha kijiji ambacho kilishuhidia maporomoko: kikiwa  cha Imonpoghet eneo la Lelan na kuripoti hakuna majerui walioripotiwa

Ningependa kuwahimiza wakazi kuhamia maeneo salama. Hawapaswi kusubiri hadi watakapokumbwa na janga,” alisema Fredrick

Mito miwili ya Konyao na Kanyangareng ilifurika kutokana na mvua iliyonyesha  Mwakilishi wadi ya Kapchok Peter Lorok alisema mifugo, mimea na miundo msingi imeathiriwa huku sehemu ya barabara inayovuka mito hiyo ikiwa haipitiki.

Mimea iliyokuwa imekuzwa kando ya mito imesowa na mafuriko huku wakaazi wa eneo hilo wakihofia kukosa chakula na pia kuadhirika na magojwa yanayosababishwa na maji chafu.

Mimea yote iliyokuwa imekuzwa kando ya mito hiyo imesombwa na mafuriko hayo huku wakazi wa eneo hilo wakiwakodolea macho na ukosefu wa chakula pamoja na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu,” alisema Lorok.


Mimea yote iliyokuwa imekuzwa kando ya mito hiyo imesombwa na mafuriko hayo huku wakazi wa eneo hilo wakiwakodolea macho na ukosefu wa chakula pamoja na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu,” aliezea Lorok.


By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE