
By Mary Amboka
Wanachama wa chama cha ushirika wa maziwa (FUNYULA DAIRY FARMERS COOPERATIVE SOCIETY) wafaidika baada ya kukabidhiwa mtambo wa kuhifadhi maziwa wa kima cha shilingi 5,000,000 kutoka kwa serikali kupitia idara ya mifugo.
Katibu katika wizara ya biashara ndogo ndogo na kadri Susan Mang’eni alitoa changamoto kwa vyama vya ushirika vinavyojihusisha na kilimo Busia kuwahusisha vijana ambao wako kwenye nafasi bora kuimarisha uchumi wa nchi kutokana na ujuzi na ubunifu walio nao.
Akizungumza na wanahabari katika soko la Funyula katika hafla ya kupeana mtambo wa kuhifadhi maziwa wa kima cha shilingi 5,000,000 kutoka kwa serikali kupitia idara ya mifugo, Susan Mang’eni aliwataka wakulima kujiunga na vyama vya ushirika ambavyo vitawawezesha kuinua mapato na kupanua soko.
Hata hivyo Bi Mang’eni alisema kuwa serikali itawahusisha vijana kikamilifu kwenye kilimo ili kuimarisha ubunifu wa kuongeza dhamana kwa lengo la kuongeza mapato zaidi kupitia kuboresha uchumi wa maeneo.
