Hali ya huzuni imetanda katika kijiji cha Mkakawai kata ndogo ya namushiya eneo bunge la Malava baada ya mwanamme mmoja mwenye umri wa makamo kupatikana akiwa amejitia kitanzi Asubuhi ya leo

Kulingana na Simbline. Barasa ambaye ni jiraniye marehemu ni kuwa alikuwa akienda mtoni kabla ya kukutana na mwili wa mwendazake Stevene Barasa Fita ukininginia juu ya mti ndani ya shamba la mahindi kando ya nyumba yake.

Ni kisa ambacho kimewatamausha wakaazi wa eneo hilo ambao wanasema kuwa marehemu hakuwa na mzozo na mtu yeyote.

Chifu wa kata ya Chegulo Juma Inzai amethibitisha kisa hicho akiwataka wananchi kutafuta ushauri nasaha wanapopitia changamoto maishani kuliko kujitoa uhai.

Mwili wa mwendazake unatarajiwa kuzikwa hapo kesho baada ya kuwepo makubaliano kati ya jamaa zake kuwa marehemu alijitoa uhai mwenyewe na wala si kuuawa.

By Imelda  Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE