Lubao FM | 102.2 Hz

  • http://41.90.240.222:88/broadwave.mp3?src=1&rate=1&ref=
  • Streaming Live

Wizi wa mifugo kukidhiri eneo la Khayega Kaunti ya Kakamega

Wakazi wa kijiji cha Sigalagala mpakani mwa eneo bunge la Shinyalu na Kakamega wameamkia kisha cha kushangaza baada watu wasiojulikana kuchinja ng’ombe na kondoo ya mmoja wa wanakijiji na kutoweka na nyama huku wakiacha ngozi, kichwa cha ng’ombe na matumbo ndani ya nyumba iliyokuwa ya marehemu mmoja kijijini.

Mmiliki wa ng’ombe huyo Josephat Mukabwa anasema aliamka asubuhi na kwenda kwa zizi la ng’ombe la kushangaza alipata kamba ya ng’ombe na kondoo zikimugodolea macho huku akibaki amedua ana kukosa la kufanya ila aliamua kuripoti kwa chifu wa Khayega kabla ya kukutana na ngozi, kichwa ya ng’ombe na matumbo ndani ya nyumba ya jamaa mmoja aliyeuawa kwa madai ya wizi na kuacha nyumba hiyo ikiwa wazi.

Wenyeji wakiongozwa na Damaris Lijoodi, Stephen Lugonzo na Muhanji Alusa wametaja visa vya wizi wa ng’ombe kukithiri kijijini wakija kisa cha hivi majuzi ambapo ng’ombe tisa za wizi zilinaswa ndani ya lori zilizokuwa zimesafirishwa kutoka mjini nakuruna mshukiwa mmoja, huku pia mwanamme mmoja akanaswa na ndama watatu wa wizi akisafirisha ndani ya tuktuk.

By Sajida Javan

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *