Mahakama mjini Sirisia imemwachilia mwanasiasa Moses Nandalwe kwa dhamana ya shilingi elfu ishirini, na mdhamini sawa na kiwango hicho baada ya kukana shtaka la kuandaa mkutano nyumbani kwake kinyume na masharti ya wizara ya afya ya kukabili msambao wa virusi vya corona ambapo kesi hiyo iliendeshwa kupitia njia ya mtandao.

Akitoa uamuzi huo hakimu George Omondi amesema uamuzi huo uliafikiwa baada ya kusikiza pande zote mbili ambapo kesi hiyo itatajwa tarehe tisa mwezi Agosti mwaka huu kabla ya kusikizwa Novemba  ishirini na mbili mwaka huu.

Nandalwe alisomewa shtaka  la kuandaa mkutano na wakaazi nyumbani kwake Sirisia tarehe kumi na tisa mwezi juni mwaka huu, kinyume na amri iliyotolewa na serikali ya kukabili msambao wa virusi vya corona, shtaka ambalo mwanasiasa huyo alikana.

Awali wakili John Makali anayemwakilisha mwanasiasa huyo  kwenye kesi hiyo alitoa sababu  za kutaka kuachiliwa mteja wake kwa dhamana, ikiwemo kufwata masharti yote yatayotolewa na mahakama hiyo.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE