Biwi la simamnzi limetanda katika kijiji cha Chongeywo kata ya Chongeywo eneobunge la Mlima Elgon baada ya mwili wa mwanamume mmoja mwenye umri wa kati kupatikana ukiwa umening’inia kwenye mti shambani.
Kulingana na Nathan Sichangi na bi Esther Sichangi ambao ni wazazi wa mwendazake Samwel Juma mwenye umri wa miaka ishirini na miwili, mwanao alikuwa na matatizo ya kiakili tangu mwezi aprili mwaka huu kabla ya kutibiwa, japo jana alionyesha dalili hizo baada ya kupata chakula cha mchana kabla kupatikana asubuhi ya leo akiwa amejitia kitanzi kwenye shamba lao.
Aidha Sichangi amedokeza kuwa mwanawe alitarajiwa kujiunga na kidato cha nne mwaka jana katika shule ya upili ya kaptanai kabla kuathirika na ugonjwa huo.
Wakaazi wa eneo hilo wakiongozwa na Noah Wokolo wakiitaka wahisani kuwapa msaada utakaofanikisha mazishi ya kijana huyo.
Chifu wa kata ya Chongeywo Eliud Kiptalaam amethibitisha tukio hilo.
By Hilary Karungani