Wito umetolewa kwa wakaazi wa kaunti ya Bungoma kukumbatia kilimo cha kisasa ili kuwaepusha na umasikini hasa baada ya kubainika kuwa kaunti hii ina ardhi yenye rotuba ya kufanikisha kilimo hicho.

Haya ni kulingana na  aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano nchini C.A.K. mhandisi Francis Wangusi ambaye amehoji kuwa kaunti hii ina rasilimali ya kutosha na kuwataka wakaazi kukumbatia kilimo cha kisasa kitakachowawezesha kukabili ukosefu wa chakula.

Vile vile wangusi amesema anajivunia kufanikisha zoezi la mawimbi ya kidigitali kwa runinga  za humu nchini na  kuhoji kuwa hatua hiyo ilipokelewa vyema na wananchi.

Hata hivyo amedokeza kuwa atabadilisha sura ya kaunti ya Bungoma iwapo wakaazi wa kaunti hii watampa nafasi ya kuhudumu kwenye wadhifa wa ugavana akisema ni sharti wakaazi wa kaunti ya Bungoma kushirikiana kikamilifu  kufanikisha ajenda ya maendeleo.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE