Wakaazi wa eneobunge la Sirisia wamehimizwa kufanya kazi kwa karibu na serikali ya kaunti ya Bungoma na ile ya kitaifa ili kuwawezesha kuzidi kunufaika na miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akihutubu kwenye hafla ya mazishi eneo la Lwandanyi mbunge wa Sirisia John Koyi Waluke amesema miradi mbalimbali ya maendeleo imetekelezwa eneo hilo baadaya kuwepo ushirikiano bora kati yake na serikali hizo mbili na kuwataka wakaazi kuiga mfano huo.

Aidha Waluke amehoji kuwa hatua ya mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Lwandanyi kwenda kinyume na sheria ya ununuzi wa bidhaa ilipelekea afisi husika kuipokonya fedha za ujenzi wa madarasa ya kisasa na kuikabidhi shule ya msingi ya Lwandanyi fedha hizo kwa lengo Sawia.

Ametumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi kujisajili katika chama cha U.D.A ili kupiga jeki azma ya naibu rais dakta William Ruto kuingia ikulu ya rais kwenye uchaguzi mkuu ujao.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE