Huku serikali ikiweka masharti ya kudhibiti msambao wa virusi vya corona baadhi ya sherehe zinazo adhimishwa kwenye hali tofauti zimewakosesha baadhi ya wakenya furaha ya kusherehekea
Ni ikiwemo sherehe ya siku ya kuzaliwa ambayo kila mmoja huadhimisha kwa kusherehekea na familia hata na marafiki
Kwa sasa hamna sherehe zinazoruhusiwa kuleta marafiki kwa pamoja kama njia moja ya kudhibiti msambao wa virusi vya corona
Hapa mwanadada Modester Alionya aliyekuwa akiadhimisha siku ya kuzaliwa anatueleza jinsi masharti hayo yalivyomkosesha raha ya kusherekea na kutoa wito kwa serikali kutadhmini upya masharti ya covid19
Hakuna aja waseme hakuna mtu kufanya sherehe ama bush kwake nyumbani na the same time watu wanaenda club wanajaa baa watu wanajaaa sijui kati ya sherehe ambazo mtu ameandaa nyumbani na kuzingatia masharti yote ya corona na kule club watu wamejaa na akuna masharti ambayo wanazingatia naomba tu serikali iweze pia kuangalia kati alafu pia tumezoea corona sai tumejua jinsi ya kujikinga mi sioni haja ya restrictions
By Sajida Javan