Na Kefa Linda

Mashindano ya riadha yaliyodhaminiwa na Profesa Fabian Makani kwa ushirikiano na Riadha ya Kenya (Athletics Kenya) yamefanyika katika Uwanja wa Chuo cha Anuwai cha Sigalagala mwaka huu, na lengo kuu likiwa ni kuendeleza talanta katika Mkoa wa Magharibi.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa mashindano hayo ambayo pia yalihusisha shule za msingi, sekondari, na za anuwai kutoka Mkoa wa Magharibi kwa wanariadha wasiozidi umri wa miaka 18, Profesa Fabian Makani, mdhamini wa mashindano hayo, ameelezea kufurahishwa na talanta ya riadha iliyopo katika Mkoa wa Magharibi na kusema lengo lake kuu ni kukuza vipaji hivyo.

Francis Afundi, Mwenyekiti wa Riadha ya Kenya Mkoa wa Magharibi, ameongeza kuwa wanaendelea kushirikiana na mdhamini huyo ili kuhakikisha talanta zinakuza kutoka chini ili wanariadha bora waendelee kutokea Mkoa wa Magharibi kuwakilisha Kenya katika mbio za masafa mafupi, huku akiwaomba wadhamini zaidi kujitokeza na kusaidia.

Naibu Mwalimu Mkuu wa Chuo cha Sigalagala, Ann Mutsami, ambaye alimwakilisha Mwalimu Mkuu Evans Bosire kwenye hafla hiyo, amepongeza juhudi za mfadhili huyo na kuelezea umuhimu wa mashindano hayo na jinsi shule yake inavyojitahidi kutambua vipaji.

Wanariadha walioshiriki katika mbio hizo wakiongozwa na Peter Wekesa kutoka Malava na Joseph Babu kutoka Vihiga walielezea jinsi walivyofaidika na mashindano hayo na kushiriki bila kukata tamaa katika kuchukua fursa ya vipaji vyao.

Hata hivyo, waligusia changamoto wanazokumbana nazo katika kukuza vipaji vyao wanapojitolea kwa mazoezi na kushiriki katika mashindano tofauti.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE