Huenda wanafunzi katika shule ya upili ya Lwanda iliyoko eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega wakalazimika kusomea chini ya miti kutokana na uhaba wa madarasa, hii ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi shuleni humo baada ya kuandikisha matokeo bora katika mtihani wa mwaka uliopita.

Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo Ferdinand Mbiti, shule hiyo imewasajili wanafunzi wengi katika kidato cha kwanza kupita matarajio yao baada ya wazazi kufurahishwa na matokeo bora ya mwaka uliopita ambapo mwanafunzi wa kwanza alipata alama ya A, jambo ambalo limesababisha msongamano wa wanafunzi katika shule hiyo.

Mbiti kwa sasa amewataka viongozi wa eneo hilo pamoja na wizara ya elimu kuingilia kati ili kutatua tatizo la uhaba wa madarasa na walimu huku ikihofiwa kuwa wanafunzi wamo katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa corona  na hata masomo kulemazwa kutokana na idadi hiyo kubwa.

By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE