Huku shule za upili kote nchini zikiendelea kupokea wanafunzi wapya, baadhi ya wazazi na wanafunzi kutoka kata ya Okuleu kaunti ndogo ya Teso kusini kaunti ya Busia, wamesalia kwenye njia panda dakika za lala salama baada ya kuachwa nje kwenye mpango wa Elimu Sacco na Wings to Fly chini ya ufadhili wa Benki ya Equity.

Wazazi hao wakiongozwa na Leonard Okeya wameambia wanahabari kuwa wanao walichaguliwa kupata ufadhili wa kimasomo na benki ya Equity, wakishangazwa na jinsi mchujo huo uliendeshwa huku wanafunzi 16 wa shule moja tu wakinufaika kati ya shule tatu zinazopatikana kata ya Okuleu.

Wanasema baadhi ya wanafunzi ambao wazazi wao wana uwezo wa kimapata wamenufaika huku wale wenye mapato ya chini wakifungiwa nje.

Wanafunzi wakielezea jinsi wamevunjwa moyo licha ya kuwa na wingi wa matumaini.

Aidha wamemtaka meneja wa benki hiyo tawi la Malaba kuelezea namna wanao walichujwa licha ya wao kuwa na matumaini makubwa, huku pia wakiwataka viongozi eneo hilo kuingilia kati.

Akijibu madi hayo meneja wa Equity tawi la Malaba Bw Boru Ali amepuunzilia mbali na kusema kwamba maafisa wake waliendesha zoezi hilo kwa mjibu wa sheria.
 By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE