Wazazi walio na watoto wenye ulemavu katika Kaunti ya Bungoma wameshauriwa kuwapeleka wanao shuleni hasa wale wanaojiunga na shule za upili, zoezi la kusajili wanafunzi wa kidato cha kwanza likiingia siku ya pili leo.

Katika shule ya upili ya watoto wenye ulemavu ya Nalondo, tayari idadi kubwa ya wanafunzi walemavu imesajiliwa kufikia sasa, hatua anayoipongeza Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Walter Kwanusu.

Mwalimu Mkuu huyo aidha amesema wanazingatia masharti ya wizara ya afya kuzuia msambao wa COVID-19 japo shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa madarasa.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE