Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 62 kutoka kijiji cha Bukati kaunti ndogo ya Butula kaunti ya Busia anauguza majeraha baada ya kupigwa na kujeruhiwa vibaya na watu sita wanaokisiwa kuwa wandani wa mbunge Joseph Oyula.

Tomas Opanyi ambaye alikuwa miongoni mwa watu waliopanga maandamano ya kumkashifu mbunge Oyula kwa kumtaka kumpokonya shamba mwanamke mmoja kwa jina Ludwina Obango, anadai aliitwa na mmoja wa wafuasi wa Oyula kwenye mkahawa mmoja katika soko la Butula kabla ya aliposhambuliwa na watu 6 wakidai anamuharibia Oyula jina.

Akizungumza na wanahabari katika hospitali ya Bumala B anakopokea matibabu, Opanyi anasema hata baada yake kukimbilia usalama katika kituo cha polisi watu hao waliendelea kumshambulia mbele ya OCS wa Butula.
Anasema licha ya vitisho msimamo wake wa kumtetea Bi Ludwina kupata haki ya shamba lake ambalo mbunge Oyula anataka kuinyakua.

Sasa anamtaka Inspekta mkuu wa polisi Hilary Mutyambai kumpa ulizi akisema maisha yake sasa yamo hatarini.  

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE